Felix Tshisekedi achaguliwa tena kuwa rais wa DRC
2024-01-01 09:14:59| CRI

Tume Huru ya Uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imesema jana kuwa, rais wa sasa wa nchi hiyo, Felix Tshisekedi, amechaguliwa tena kuongoza nchi hiyo kwa kipindi cha pili cha miaka mitano baada ya kupata asilimia 73.34 ya kura zote zilipopigwa katika uchaguzi uliofanyika Desemba 20 mwaka jana.

Tume hiyo imesema, zaidi ya watu milioni 18 kati ya jumla ya watu milioni 44 waliojiandikisha kupiga kura, walitimiza haki yao hiyo ya kikatiba.

Rais mteule Tshisekedi anatarajiwa kuapishwa tarehe 20 mwezi huu, baada ya Mahakama ya Katiba kuthibitisha matokeo ya uchaguzi tarehe 10 mwezi huu.

Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi ya nchini DRC, katika uchaguzi huo, Moise Katumbi, mmoja wa wagombea wakuu kutoka upande wa upinzani, alichukua nafasi ya pili kwa kupata asilimia karibu 18 ya kura zote.