Kamanda mkuu wa jeshi la Sudan alitaka jeshi la RSF liondoke kutoka miji yote ili kutimiza usitishaji wa mapambano
2024-01-01 09:58:57| cri


 


Mwenyekiti wa Baraza la Mpito la Sudan ambaye pia ni kamanda mkuu wa jeshi la Sudan (SAF) Jenerali Abdel Fattah Al-Burhan amesema, usitishaji wa mapambano hautatimizwa mpaka pale kikosi cha Mwitikio wa Haraka (RSF) kitakapoondoka kutoka miji yote, nyumba za raia na makao makuu ya serikali.

Akizungumza kwenye hafla ya maadhimisho ya miaka 68 ya uhuru kwa Sudan jumamosi iliyopita, Jenerali Al-Burhan amesema, usitishaji wowote wa mapambano usiohakikisha kutimizwa kwa masharti yaliyotajwa hautakuwa na thamani, na wananchi wa Sudan hawatakubali kuishi miongoni mwa wauaji, wahalifu na wale wanaowaunga mkono.