Mkuu wa CMG atoa salamu za mwaka mpya wa 2024
2024-01-01 15:11:54| CRI

Leo ni tarehe Mosi Januari mwaka 2024. Katika kusherehekea mwaka mpya, Mkuu wa Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) Shen Haixiong ametoa salamu za mwaka mpya wa 2024 kupitia Shirika la Kimataifa la Televisheni la China, Radio China Kimataifa na mtandao wa Internet. Ifuatayo ni hotuba hiyo:

Wapendwa marafiki,

Wakati tunapokaribisha miale ya kwanza ya jua katika mwaka mpya, tumeingia mwaka 2024 wenye matumaini mengi. Ninawasalimieni kutoka Beijing!

Katika mwaka uliopita, Pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” limetimia kipindi cha kwanza cha miaka 10 chenye ustawi mkubwa, na kupata mafanikio mengi, na China imesonga mbele pamoja na nchi nyingine duniani. Katika mchakato huo, CMG imeendelea kuhimiza mawasiliano ya staarabu mbalimbali, na kurekodi hadithi nyingi za kugusa moyo duniani.

Katika mwaka uliopita, CMG imeinua zaidi kiwango cha uvumbuzi wa kuunganisha mawazo, usanii na teknolojia. Kipindi cha Pili cha Hadithi za Kihistoria zinazopendwa na Rais Xi Jinping kimetolewa kwa lugha mbalimbali kupitia televisheni katika zaidi ya nchi 80 duniani. Vipindi vingine vizuri vya “Maendeleo ya Utamaduni”, “China ya Kale”, “Kukutana kwa Staarabu” na “Fahamu China Kupitia Vitabu” vimeonesha nuru ya ustaarabu wa China na staarabu nyingine duniani. Aidha, vipindi vya CMG kuhusu Michezo ya Asia ya Hangzhou vilitazamwa mara bilioni 41.4, na kuvunja rekodi katika historia.

Katika mwaka uliopita, urafiki umeimarishwa. Licha ya marafiki zetu wakubwa, pia tumekuwa na wenzi wapya. Tumesaini makubaliano 58 ya ushirikiano na vyombo vya habari vya kimataifa, na pia tumeandaa Kongamano la Pili la Uvumbuzi wa Vyombo vya Habari Duniani, Kongamano la Ushirikiano wa Vyombo vya Habari kati ya China na ASEAN, na Kongamano la Ushirikiano wa Vyombo vya Habari kati ya China na Afrika. Zaidi ya hayo, pia tumeandaa mikutano 51 ya vyombo vya habari kuhusu “Utimizaji wa Mambo ya Kisasa Nchini China na Dunia”, maonesho 8 ya “Ustaarabu ni Nini”, ili kuchora picha nzuri ya dunia yenye maendeleo ya amani, ushirikiano wa kunufaishana, na ustawi wa pamoja.

Dunia ya leo bado haijatimiza amani, na inahitaji sana amani, maendeleo, ushirikiano na mafanikio ya pamoja! Jambo linalotufurahisha ni kwamba, marafiki wengi zaidi wamefahamu, kukubali na kuunga mkono mawazo na mapendekezo ya China. Katika mkutano wa APEC uliofanyika nchini Marekani, tuliandaa “Mazungumzo ya Kirafiki ya Mawasiliano ya Watu kati ya China na Marekani,” na kupata mwitikio mkubwa. Bw. Harry Moyer mwenye umri wa miaka mia moja, aliyekuwa askari wa Kikosi cha Flying Tigers cha Marekani kilichosaidia China kupambana na wavamizi wa Japan wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia, pia alihudhuria mazungumzo hayo. Aliniambia kuwa dhana ya Rais Xi ya jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja inakubaliwa na watu wengi. Baada ya kurudi nchini China, nilipata zawadi mbalimbali zilizotengenezwa na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Lincoln ya Marekani ikiwemo postikadi, globu ya dunia, na mapambo madogo, ambazo zilinifanya nihisi hamu ya watoto hao kwa amani, urafiki, na ustawi wa pamoja.   

Likiwa shirika kubwa zaidi la vyombo vya habari duniani, hadi sasa Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) limetimiza miaka mitano, na limepita safari ya kujiendeleza ya kutoka shirika chipukizi kuwa jukwaa kubwa lenye ushawishi. Mwaka jana, tulikamilisha ujenzi wa kituo cha 191 nje ya nchi, kuanzisha mtandao wa utangazaji katika nchi na sehemu 67 duniani. Idadi ya watumiaji wa Mtandao wa Televisheni wa Kimataifa wa China (CGTN) nje ya nchi imezidi milioni 700 kwa mara ya kwanza, na shirika letu mara nyingi limekuwa chanzo cha habari muhimu duniani. Katika safari ya kujijenga kuwa chombo cha habari cha hali ya juu na cha aina mpya duniani, tutaendelea kuharakisha hatua za kujiendeleza kwa lengo la “kuandaa vipindi bora”.

Wapendwa marafiki, mwaka 2024 ni Mwaka wa Dragoni katika Kalenda ya Jadi ya Kichina. Dragoni ambaye ni mnyama wa kufikirika katika hadithi za kufikirika nchini China, anaashiria bahati nzuri na neema, anawakilisha roho ya kukusanya nguvu za viumbe wote, kunufaisha vitu vyote, kutafuta msingi wa usawa wakati wa kupunguza tofauti, na kutafuta masikilizano ya kutoka mbinguni hadi ardhini. Watu wa China wanaosonga mbele katika safari mpya ya maendeleo, watakaribisha miaka 75 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China katika Mwaka wa Dragoni. CMG itaenzi moyo wa Dragoni ambao ni busara na ushupavu, kutangaza hadithi nyingi zaidi za China na dunia, kuandika kurasa za kisasa za ustaarabu wa binadamu, na kukaribisha msimu mpya wa Mchipuko kwa pamoja.

Nawatakieni ninyi na dunia baraka, heri ya Mwaka Mpya!