ATMIS yatoa kipaumbele katika kulishinda kundi la al-Shabab mwaka huu wa 2024
2024-01-01 09:14:09| CRI

Tume ya Mpito ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS) imesema, katika mwaka huu wa 2024, kipaumbele chake kitakuwa kulisambaratisha kundi la al-Shabab na kuboresha uwezo wa Vikosi vya Usalama vya Somalia.

Kamanda wa Tume hiyo, na Kamishna wa Polisi Hillary Sao Kanu amesema hayo alipotoa hotuba ya mwisho wa mwaka hapo jana, ambapo pia alisema operesheni za usalama zitaongezwa nchini kote. Amesema mkutano utakaokutanisha makamanda wa sekta zote za Tume hiyo utafanyika mjini Mogadishu ili kuhakiki Dhana ya sasa ya Operesheni ili kukabiliana kwa ufanisi na vita dhidi ya kundi la al-Shabab.

Amesema kuwa operesheni hizo ni muhimu katika kulinda vituo vya umma, kulinda njia kuu za ugavi, kukomboa miji na vijiji muhimu, na kuwezesha usambazaji wa msaada wa kibinadamu kwa jamii zilizo hatarini.