Idadi ya vifo vilivyotokana na mafuriko nchini Afrika Kusini yafikia 22
2024-01-01 09:07:41| cri

Idara ya Utawala Bora na Masuala ya Kitamaduni ya mkoa wa KwaZulu-Natal nchini Afrika Kusini imesema, idadi ya watu waliofariki kufuatia mafuriko ya ghafla yaliyotokea hivi karibuni katika mkoa huo, imeongezeka na kufikia 22, na wengine watatu bado hawajulikani walipo.

Mvua kubwa iliyonyesha tarehe 24, mwezi wa Desemba mwaka jana ilisababisha Mto Bellspruit kuvunja kingo zake, na kusababisha mafuriko kwenye barabara ya 11 katika Mji wa Ladysmith, Mkoa wa KwaZulu-Natal. Mafuriko hayo pia yalisomba magari kadhaa yaliyokuwa yakisafiri katika barabara hiyo na nyumba zilizokuwa karibu na barabara hiyo.