Zambia yarekodi kesi mpya 189 za kipindupindu ndani ya siku moja
2024-01-01 09:15:34| CRI

Zambia imerekodi kesi mpya 189 za kipindupindu na vifo vya watu wanane katika saa 24 zilizopita, wakati ugonjwa huo ukienea katika wilaya nyingine zaidi.

Katika ripoti yake mpya, Wizara ya Afya nchini humo imesema, jumla ya kesi za ugonjwa huo tangu ulipolipuka mwezi Januari mwaka jana mpaka sasa ni 3,702, huku idadi ya vifo ikiongezeka na kufikia 105.

Jumla ya watu 150 waliruhusiwa kutoka hospitali katika saa 24 zilizopita na wengine 245 bado wamelazwa katika vituo mbalimbali vya matibabu.