Idadi ya vifo vya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza yafikia 21,978
2024-01-02 08:29:01| cri

Wizara ya Afya inayoongozwa na kundi la Hamas la Palestina imesema, idadi ya Wapalestina waliouawa tangu kuzuka kwa mapigano kati ya Israel na Palestina tarehe 7 Oktoba mwaka jana imefikia 21,978.

Msemaji wa Wizara hiyo Bw. Ashraf al-Qedra amesema jana kuwa, katika saa 24 zilizopita, Wapalestina 156 wameuawa na wengine 246 kujeruhiwa katika Ukanda wa Gaza.

Bw. al-Qedra pia amesema, mashambulizi ya Israel yamesababisha vifo vya wahudumu wa afya 326 na kulazimu hospitali 30 kati ya 35 za Ukanda wa Gaza kushindwa kutoa huduma.