Wizara ya Mambo ya Nje ya China yazungumzia maadhimisho ya miaka 45 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Marekani
2024-01-02 16:51:17| CRI

China na Marekani mwaka huu zinaadhimisha miaka 45 ya uhusiano wa kidiplomasia, ambapo hapo jana tarehe mosi, rais Xi Jinping wa China na mwenzake Joe Biden walipeana barua za pongezi kwa ajili ya maadhimisho haya.

Ikizungumzia maadhimisho hayo, wizara ya mambo ya nje leo imesema kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Marekani ni tukio muhimu katika historia ya uhusiano kati ya nchi hizi mbili na uhusiano wa kimataifa. Kwa miaka 45, uhusiano kati ya China na Marekani umekabiliana na panda shuka nyingi na kufika hapa ulipo sasa.

Kuhusu biashara baina ya nchi mbili, wizara hiyo imesema ilipanda kutoka chini ya dola bilioni 2.5 mwaka 1979 hadi kufikia dola bilioni 760 mwaka 2022, ambapo uwekezaji wa pande mbili uliongezeka kutoka karibu sifuri hadi zaidi ya dola bilioni 260. Nchi hizo mbili pia zimefanya ushirikiano muhimu katika maeneo muhimu ya kimataifa na kikanda na masuala ya kimataifa.

Wizara pia imebainisha kuwa historia inaonesha kukua kwa uhusiano kati ya China na Marekani sio tu kunachangia manufaa ya watu wa nchi hizo mbili bali pia amani, utulivu na maendeleo ya dunia.