IMF: Tanzania miongoni mwa nchi zinazokua kwa kasi kiuchumi mwaka 2024
2024-01-02 11:09:40| cri

Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limetabiri kuwa Tanzania itakuwa na ukuaji wa kasi wa uchumi kwa mwaka 2024. Tanzania ni miongoni mwa nchi 12 za Afrika na 22 duniani kote katika nafasi ya juu katika ukuaji wa uchumi kwa mwaka huu. Ndani ya Afrika Mashariki, Tanzania inawekwa kundi moja na Ethiopia, zote mbili zinatarajiwa kuvutia uwekezaji zaidi kutoka nje.

Tanzania na Ethiopia zinabadilika kuwa nchi zenye ukuaji mzuri wa uchumi katika eneo la Afrika kusini mwa Sahara. Uzalishaji wa ndani na maendeleo ya viwanda vimetajwa kuwa vichocheo muhimu vya ukuaji chanya katika nchi hizo mbili.

Kwa mujibu wa shirika hilo, makadirio ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania na Ethiopia mwaka 2024 ni asilimia 6.1 na 6.2 mtawalia.