Zaidi ya kesi 14,000 za homa ya dengue zaripotiwa nchini Ethiopia
2024-01-02 08:31:55| criShirika la Afya Duniani (WHO) jana limesema, kesi 14,249 za homa ya dengue zimeripotiwa nchini Ethiopia katika mwaka 2023.

Katika ripoti yake ya hali ya dharura ya afya barani Afrika, WHO imesema, zaidi ya watu 7 wamefariki nchini Ethiopia kutokana na homa ya dengue.

Shirika hilo pia limesema, hivi sasa linaisadia Ethiopia kuchukua hatua za kukabiliana na ugonjwa huo, ikiwa ni pamoja na uratibu, ujenzi wa uwezo, ugunduaji wa kesi, udhibiti wa vijidudu, usimamizi wa kesi na uhamasishaji wa kijamii.