Iran yasema ina haki ya kulipiza kisasi kufuatia mauaji ya kamanda wa IRGC
2024-01-02 08:33:03| CRI

Iran imesema kuwa ina haki ya kulipa kisasi kutokana na mauaji ya kamanda wa nchi hiyo nchini Syria katika sehemu na muda sahihi.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Nasser Kanaani amesema hayo katika mkutano wake na wanahabari uliofanyika Teheran, akiilaani Israel kwa kumshambulia kamanda wa Jeshi la Ulinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) ambaye alikuwa mjini Damascus kupambana na ugaidi kutokana na ombi la serikali ya Syria.

Kauli ya Kanaani imekuja wiki moja baada ya Seyyed Razi Mousavi, aliyekuwa akihudumu kama mshauri wa kijeshi nchini Syria, kuuawa kutokana na shambulio la kombora mjini Damascus Desemba 25 mwaka jana.