Ushirikiano wa China na Ethiopia unaendelea kwa kasi katika sekta mbalimbali
2024-01-02 08:32:18| CRI

Balozi wa China nchini Ethiopia Zhao Zhiyuan amesema, ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika maeneo mbalimbali umeendelea kushika kasi.

Katika waraka wake wa kukaribisha mwaka mpya uliochapishwa na Shirika la Habari la Ethiopia (EPA) jumapili iliyopita, Balozi Zhao alisisitiza kuwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili utaendelea kupanuka katika mwaka huu mpya. Amesema pande hizo mbili zitaendelea kupata maendeleo katika ushirikiano wa kivitendo katika biashara, uwekezaji, miundombinu, kilimo, mawasiliano, fedha, utamaduni, elimu, mawasiliano ya watu na watu, na katika maeneo mengine, na kuleta manufaa zaidi kwa watu wa nchi hizo.

Pia amesema, China na Ethiopia zimeinua ngazi ya uhusiano wa pande mbili kuwa uhusiano wa kina wa pande zote, ikimaanisha kuwa, nchi hizo zimekubaliana kuongeza uungaji mkono katika masuala ya maslahi ya kila upande na yanayofuatiliwa kwa pamoja.