Watu 57 wafariki katika tetemeko la ardhi la Peninsula ya Noto, Japan
2024-01-03 09:06:55| cri

Takwimu zilizotolewa mamlaka nchini Japan, zinaonesha kuwa tetemeko la ardhi lililotokea kwenye Peninsula ya Noto limesababisha vifo vya watu 57.

Wizara ya Ulinzi ya Japan imesema, askari 1,000 wa Kikosi cha Kujilinda cha nchi hiyo wamekuwa wakifanya shughuli za uokoaji katika maeneo yaliyokumbwa na maafa. Katibu mkuu wa baraza la mawaziri la Japan Bw. Yoshimasa Hayashi amesema, hadi kufikia jana idadi ya watu wanaotafuta hifadhi katika mikoa ya Ishikawa na Niigata ilikaribia 60,000.

Idara ya zimamoto ya Japan pia imesema zaidi ya watu 100 kote nchini Japan wamejeruhiwa kutokana na tetemeko hilo.

Mamlaka ya Hali ya Hewa ya Japan ilitabiri kuwa mvua itaanza kunyesha katika mkoa wa Ishikawa usiku wa tarehe 2, na wakazi wa eneo hilo lazima wachukue tahadhari dhidi ya maporomoko ya udongo.