Chama cha Hezbollah cha Lebanon tarehe 2 Januari usiku kilitoa taarifa kikisema makamu mwenyekiti wa ofisi ya siasa ya kundi la Hamas Saleh Al-Arouri alishambuliwa na kuuawa kusini mwa Beirut. Tukio hilo ni kitendo cha shambulizi dhidi ya mamlaka ya Lebanon na usalama wa watu wa nchi hiyo, na kwamba mauaji ya Al-Arouri yana athari kubwa ya kisiasa na kiusalama, pia ni “maendeleo ya mwelekeo wa hatari” kwenye mchakato wa mapambano na Israel.
Taarifa hiyo imesema tukio hilo la shambulizi litajibiwa, kwani jeshi la Chama cha Hezbollah limefanya maandalizi ya kutosha.