Wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa yatangaza kufunga ubalozi wake nchini Niger
2024-01-03 09:06:20| criWizara ya mambo ya nje ya Ufaransa imetoa taarifa ikisema inafunga ubalozi wake nchini Niger.

Wizara hiyo imesema tangu mapinduzi ya kijeshi yatokee nchini Niger miezi mitano iliyopita, ubalozi wa Ufaransa nchini Niger umekabiliwa na “vizuizi vikubwa” kama vile vizuizi vya kusafiri na kufukuzwa kwa wafanyakazi wa kidiplomasia, na haujaweza kuendelea na kazi yake. Taarifa hiyo imesema ubalozi huo utaendelea na kazi yake huko Paris, wakati huo huo utadumisha mawasiliano na wafaransa nchini Niger na mashirika ya kiraia yanayoshughulikia mambo ya utoaji wa misaada ya kibinadamu.