Ethiopia yasema iko tayari kuchukua jukumu la kujenga kama mwanachama mpya wa BRICS
2024-01-03 09:19:06| CRI

Serikali ya Ethiopia imeeleza utayari wake wa kuchukua jukumu la kujenga utaratibu wa BRICS wakati inaanza uanachama katika kundi la BRICS.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Ethiopia, inasema uanachama wake katika familia ya BRICS umeonesha dhamira ya nchi hiyo ya Afrika Mashariki katika mfumo wa Ushirikiano wa Kusini- Kusini.

Taarifa imesema uamuzi wa kihistoria wa kuialika Ethiopia kujiunga na mfumo wa BRICS umetambua hali ya sasa na uwezo wa uchumi wa Ethiopia ambao unafanyiwa mageuzi.

Taarifa pia imesema Ethiopia ikiongozwa na kanuni zake za muda mrefu na historia tajiri ya ushirikiano wa pande nyingi, inaendelea kujitolea na kuwa tayari kuchukua jukumu la kuhimiza amani na ustawi ikiwa mwanachama mpya wa familia ya BRICS kwa ushirikiano na wanachama wake wote.