Uwekezaji wa China waimarisha uendelezaji wa nishati mpya nchini Zimbabwe
2024-01-03 09:09:37| CRI

Waziri wa Maveterani wa Zimbabwe Bw. Christopher Mutsvangwa amesema, utaalamu wa China katika teknolojia ya nishati mpya na uwekezaji wa makampuni yake nchini Zimbabwe unahimiza nchi hiyo kuwa mshiriki muhimu katika mageuzi ya kijani duniani.

Waziri huyo amesema Zimbabwe inatumia uwezo wa kiviwanda wa China kuhimiza mageuzi ya nishati mpya duniani, na kwamba inakaribisha uwekezaji kutoka China.

Bw. Mutsvangwa amesema kutokana na miradi mikubwa ya uchakataji wa madini ya lithium iliyowekezwa na China, Zimbabwe inapiga hatua ya kuonesha jukumu kubwa katika mnyororo wa thamani ya lithiamu duniani.

Mwezi Desemba mwaka jana, serikali ya Zimbabwe ilipiga marufuku uuzaji wa lithium ghafi nje ya nchi, ili kuhamasisha uwekezaji katika miundo mbinu ya viwanda vya uchakataji ya huko. Pia iliidhinisha sera ya madini ya lithium ili kuimarisha mkakati wa madini wa nchi hiyo.