Wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa yatangaza kufunga ubalozi wake nchini Niger
2024-01-03 23:31:32| cri

Wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa imetoa taarifa kuwa itafunga ubalozi wake nchini Niger.

Wizara hiyo imesema ubalozi huo utaendelea kufanya kazi husika mjini Paris na pia utadumisha mawasiliano na wafaransa nchini Niger na mashirika yasiyo ya kiserikali katika sekta ya misaada ya kibinadamu.

Mapinduzi ya kijeshi yalitokea nchini Niger mwezi Julai mwaka jana na balozi wa Ufaransa nchini Niger Sylvain Itte aliondoka nchini humo mwezi Septemba mwaka huo.