Rais wa UAE afanya mazungumzo na mkurugenzi mkuu wa WHO
2024-01-03 14:25:18| cri

Tarehe 2 Januari rais Mohamed bin Zayed Al Nahyan wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) alifanya mazungumzo na mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya duniani (WHO) Bw. Tedros Adhanom Ghebreyesus.

Pande hizo mbili zilijadili kuhusu ushirikiano kati ya UAE na WHO katika sekta mbalimbali na matatizo ya kiafya yaliyopo yanayoukabili ukanda wa Gaza. Pande hizo mbili pia zimesisitiza haja ya kutoa msaada wa matibabu unaohitajika kwa watu wa Gaza na kuhakikisha kwamba utoaji wake hauna vikwazo vyovyote.

Mohammed alisema UAE imejitolea kuimarisha ushirikiano wake na WHO ili kuimarisha jukumu lake muhimu la kuwahudumia watu duniani kote. Bw. Tedros ameshukuru juhudi za UAE katika kutoa msaada wa kibinadamu na kiafya kwa Ukanda wa Gaza.