Kikosi cha RSF cha Sudan chasaini azimio na kundi la kisiasa la Sudan mjini Addis Ababa, Ethiopia
2024-01-03 14:32:10| cri

Kikosi cha Msaada wa Haraka cha Sudan (RSF) kimesaini azimio na Shirika la Uratibu wa Vikosi vya Kidemokrasia vya Kiraia (the Coordination of Civil Democratic Forces), kundi la kisiasa la Sudan, katika mji wa Addis Ababa nchini Ethiopia.

Azimio hilo limesema kikosi hicho kimekubali kufanya mazungumzo na jeshi la Sudan kuhimiza pande hizo kukomesha mapigano kati yao na kufikia amani ya kudumu nchini humo. Pia kikosi hicho kimeahidi kufungua njia ya upatikanaji wa misaada ya kibinadamu na kutoa urahisi na uhakikisho wa usalama kwa kazi ya utoaji wa misaada na wafanyakazi husika.

Shirika la Uratibu wa Vikosi vya Kidemokrasia vya Kiraia limetangaza siku hiyo kwamba Kamanda Mkuu wa Jeshi la Sudan Jenerali Abdel Fattah Al-Burhan amekubali kukutana na kiongozi cha shirika hilo ambaye pia ni waziri mkuu wa zamani wa serikali ya mpito ya Sudan Bw. Abdalla Hamdok, ila muda na sehemu ya kukutana bado havijathibitishwa.