Malipo ya simu yapungua kwa mara ya kwanza nchini Kenya
2024-01-04 22:49:07| cri

Kwa mara ya kwanza peza zinazotumwa na kupokelewa kwa simu nchini Kenya zilipungua mwaka wa 2023 kutokana na hali ngumu ya maisha. Takwimu kutoka kwa benki kuu ya Kenya CBK, zilonyesha kuwa kwa mara ya kwanza tangu huduma ya kutuma na kupokea pesa kuanza kutumiwa nchini Kenya miaka 17 iliyopita, kiwango cha pesa hizo kilipungua huku mwezi Novemba ukirekodi upungufu mkubwa wa pesa zilizotumwa na kupokelewa kwa simu. 

Tangu mwaka wa 2007 wakati huduma ya kutuma na kupokea pesa kwa njia ya simu ilizinduliwa na kampuni ya mawasilino ya Safaricom, kiwango cha miamala sawa na wateja kimekuwa kikiongezeka mwaka hadi mwaka ila mwaka 2023 mambo yalikuwa tofauti. Baadhi ya wachanganuzi wa masuala ya kiuchumi nchini Kenya wamesema kuongezwa kwa ushuru wakati wa kufanya miamala kwa njia ya simu na gharama ya juu ya maisha ni sababu ambazo zimewafanya Wakenya kupunguza matumizi ya simu kufanya biashara.