AU yalaani shambulizi la kigaidi nchini Burundi
2024-01-04 09:02:09| CRI

Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AU) Bw. Moussa Faki amelaani shambulizi la kigaidi lililotokea hivi karibuni nchini Burundi.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Bw. Faki amesema anasikitishwa na shambulizi hilo la kigaidi lililotokea katika Kituo cha mpakani cha Vugizo kwenye mkoa wa Gatumba nchini Burundi.

Pia amesema anaunga mkono juhudi zote za kitaifa na kikanda zinazolenga kuwakamata na kuwafikisha mbele ya sheria wahusika wa shambulizi hilo.

Bw. Faki vilevile amesisitiza AU itaendelea kutekeleza ahadi yake ya kujikita katika mapambano dhidi ya ugaidi katika Afrika ya Kati na nchi za eneo la Maziwa Makuu.