Tetemeko kubwa la ardhi la Japan lazua wasiwasi wa usalama wa nyuklia
2024-01-04 09:04:30| CRI

Tetemeko kubwa la ardhi lililotokea Jumatatu katikati mwa Japani, limesababisha wasiwasi juu ya usalama wa vinu vya nyuklia katika eneo lililoathiriwa na tetemeko.

Msururu wa matetemeko makali, ambapo kubwa kabisa lilikuwa na kipenyo cha 7.6 kwenye kipimo cha richta, yalipiga kwenye Peninsula ya Noto katika mkoa wa Ishikawa siku ya Jumatatu. Mamlaka ya Hali ya Hewa ya Japani imeliita rasmi Tetemeko la Ardhi la 2024 Noto Peninsula. Kwa mujibu wa shirika la utangazaji la umma la Japan NHK, takriban watu 73 wamefariki kwenye tetemeko hilo.

Kufuatia tetemeko la ardhi la ukubwa wa 7.6, wasiwasi uliibuka juu ya usalama wa nyuklia nchini Japan, ambao umekuwa ukitiliwa shaka mara kwa mara tangu tetemeko la ardhi na tsunami ya mwaka 2011 ambayo ilisababisha kuharibika kwa kinu cha nyuklia cha Fukushima.