Mkurugenzi wa IMF aonya kuwa mpasuko wa kiuchumi wa dunia utasababisha hasara kubwa
2024-01-04 09:02:12| criMkurugenzi wa Shirika la fedha duniani (IMF) Bi.Kristalina Georgieva hivi karibuni alionya kuwa mpasuko wa kiuchumi wa dunia huenda ukasababisha hasara ya asilimia 7 ya jumla ya mapato ya kitaifa ( (GDP) duniani.

Bi. Georgieva alisema vizuizi kuhusu “usalama wa taifa” vinaongezeka, na mambo ya siasa za kijiografia yanasababisha mpasuko wa kiuchumi. Kama mpasuko huu ukiendelea, jumla ya mapato ya kitaifa itapungua kwa asilimia 7, ambayo ni sawa na thamani ya jumla ya GDP ya nchi mbili za Ufaransa na Ujerumani.