Tanzania kuanza kuuza maparachichi China
2024-01-04 09:50:32| cri

Wakulima wa maparachichi nchini Tanzania wataanza kuuza zao hilo nchini China hivi karibuni baada ya mamlaka ya forodha ya China GACC kutoa kibali kwa mashamba mamatu ya parachichi nchini Tanzania kuanza kusafirisha parachichi hadi China.

Mashamba hayo matatu, ikiwa ni pamoja na shamba la Rutuba eneo la Arusha, shamba la Africado mkoani Kilimanjaro na lile la Usa mjini Arusha yatakaguliwa kwa njia ya video mwezi Machi mwaka huu kabla ya kuanza usafirishaji wa matunda hayo kuelekea China. 

Hii itakuwa hatua kubwa katika mpango wa serikali ya Tanzania kupata dola bilioni mbili kila mwaka kutokana na mauzo ya mboga, maua na matunda nje ya nchi. Kadhalika, wakulima wa Tanzania wanatarajiwa kuongepa pato lao kutokana na biashara hii.