Ongezeko la bajeti ya kijeshi ya Marekani latishia amani duniani
2024-01-04 08:53:59| Cri

Hivi karibuni serikali ya Marekani ilitangaza bajeti ya matumizi ya kijeshi kwa mwaka 2024 ya dola bilioni 886 za kimarekani, na kuongezeka kwa karibu dola bilioni 30 ikilinganishwa na mwaka jana, na kuvunja rekodi ya historia tena.

Katika miaka ya hivi karibuni, ili kudumisha umwamba wake duniani, Marekani imeendelea kuongeza bajeti yake ya kijeshi. Katika mwaka wa fedha wa 2024, matumizi ya kijeshi ya Marekani ni pamoja na dola bilioni 37.7 kwa ajili ya kuendeleza makombora mapya, ndege ya kimkakati ya kutupa mabomu na silaha za nyuklia, dola bilioni 170 kwa ununuzi wa silaha nyingine za kisasa, na dola bilioni 145 kwa maendeleo ya makombora ya kasi kubwa. Wakati huo huo, serikali ya Marekani tayari imekumbwa na mizigo mikubwa ya madeni, na madeni yake ya jumla yatazidi dola trilioni 31 za kimarekani. Matumizi makubwa mno ya kijeshi bila shaka yataathiri maendeleo ya uchumi na maisha ya watu. Kulingana na matokeo ya kura za maoni zilizotolewa na vyombo vya habari vya Marekani hivi karibuni, asilimia 69 ya Wamarekani wanaona kuwa nchi yao iko katika mdororo wa kiuchumi, na asilimia 55 ya watu walisema watapoteza kila kitu.

Katika miongo kadhaa iliyopita, Marekani imekuwa nchi yenye bajeti kubwa zaidi ya kijeshi duniani, na matumizi yake ya kijeshi yanachukua takriban asilimia 40 ya matumizi ya jumla ya kijeshi ya nchi zote duniani. Kuanzia mwaka 1789 hadi 2022, Marekani ilifanya vita na operesheni 469 za kijeshi duniani. Katika historia ya zaidi ya miaka 240 ya Marekani, kumekuwa na miaka 16 tu bila ya vita. Baada ya kumalizika kwa Vita Baridi, Marekani ilitarajiwa kupunguza operesheni zake za kijeshi nje ya nchi, lakini kinyume chake, katika miaka zaidi ya 30 iliyopita Marekani imefanya operesheni zaidi ya mara saba kuliko zamani. Vita vya Marekani vimelenga nchi mbalimbali duniani, haswa nchi za Latin-Amerika, na Afrika.

Baada ya kumalizika kwa Vita Vikuu vya Pili Duniani, ili kutimiza maslahi yake ya kijiografia na kisiasa, Marekani mara kwa mara ilichochea migogoro duniani kwa kutegemea bajeti yake kubwa ya kijeshi. Kwa nyakati tofauti ilianzisha vita vikubwa katika peninsula ya Korea, Vietnam. Iraq, Afghanistan, Libya, Syria na nchi nyingine kadhaa. Mbali na hayo, Marekani pia imechochea migogoro katika nchi nyingi duniani. Takwimu zinaonesha kuwa takriban theluthi mbili ya mizozo ya hivi sasa duniani inahusisha Marekani. Tangu kutokea kwa mgogoro kati ya Russia na Ukraine, Marekani imetoa silaha nyingi, na kuongeza umwagaji damu kwa kiasi kikubwa. Wakati China ilionesha nia ya kusuluhisha mgogoro huo, Marekani imekataa kabisa, ikijifanya kama mhusika mkuu wa mgogoro huo, na kutaka vita kati ya Russia na Ukraine viendelee mpaka iridhike.