Bei Ya Mafuta Yashuka Dizeli, Petroli Kutumika Kuanzia Januari 03, 2024 Tanzania
2024-01-04 22:18:33| cri

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji Tanzania (EWURA), imetangaza kushuka kwa bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli nchini Tanzania zilizoanza kutumika kuanzia Jumatano Januari 3, 2024 ambapo sasa bei ya petroli ni Tsh. 3084 kwa lita, dizeli Tsh. 3078 na mafuta ya taa 3510.

Mamlaka hiyo imesema kupungua kwa bei za mafuta kwa mwezi Januari 2024, kwanza ni kwa sababu ya kushuka kwa bei za mafuta (FOB) katika soko la dunia kwa wastani wa asilimia 6.03 kwa petroli na asilimia 7.13 kwa dizeli, na pia kushuka kwa gharama za uagizaji wa mafuta kwa bandari za Dar es Salaama na Mtwara.

EWURA pia imewakumbusha wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta kwa rejareja kuuza mafuta kwa bei mpya, na kwamba hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wafanyabiashara watakaokiuka agizo hilo.