Rais wa zamani wa Sierra Leone Koroma ashtakiwa kwa uhaini
2024-01-04 09:09:54| cri

Serikali ya Sierra Leone jana ilitangaza kwamba, rais wa zamani wa nchi hiyo Bw. Ernest Bai Koroma anashukiwa kushiriki katika jaribio la mapinduzi na anashtakiwa kwa uhaini.

Wizara ya Habari na Elimu ya Umma ya Sierra Leone ilitoa taarifa siku hiyo ikisema kuwa, Bw. Koroma anakabiliwa na mashtaka manne yakiwemo ya uhaini na kuhifadhi. Taarifa hiyo haikufafanua zaidi, lakini ilisema kuwa habari muhimu kuhusu kesi hiyo itawekwa wazi kwa umma kwa wakati ufaao.

Habari zinasema, mapema asubuhi ya tarehe 26. Novemba, kundi la wanamgambo wasiojulikana walishambulia ghala la silaha na gereza katika kambi ya kijeshi huko Freetown, mji mkuu wa Sierra Leone, na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 20 na kutoroka kwa idadi kubwa ya wafungwa.