Serikali ya Uganda kufadhili bajeti yake kwa mikopo ya ndani
2024-01-04 09:51:00| cri

Serikali ya Uganda inatarajiwa kufadhili bajeti yake yake kutokana na pesa inazokopa ndani ya nchi baada ya a ufadhili wa kimataifa kupungua zaidi.

Kulingana na wachanganuzi wa masuala ya kiuchumi nchini Uganda, hali hii itaendelea hadi  wakati uagizaji wa mafuta kutoka nje utapungua na mapato ya mafuta kuongezeka.

Takwimu kutoka kwa  Mamlaka ya Uwekezaji ya Uganda na Benki ya Uganda, zinaeleza kuwa mwaka 2023 Uganda ilirekodi  ukuaji wa asilimia 20 katika mapato ya kigeni, sehemu kubwa ya fedha hizo zikitokana na biashara ya mafuta.