Mwaka Mpya wa Jadi wa Kichina kuwa sikukuu ya kimataifa
2024-01-04 08:52:55| Cri

Mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hivi karibuni umepitisha kwa kauli moja azimio la kuweka Mwaka Mpya wa Jadi wa China kuwa sikukuu ya Umoja huo. Kwa miaka mingi, Katibu Mkuu wa Umoja huo ametoa salamu za pongezi kila Wachina wanaposherehekea Mwaka Mpya wa Jadi wa China, na kuwatakia kila la heri. Wakati huohuo viongozi wa nchi mbalimbali duniani pia hutoa salamu za mwaka mpya kwa Wachina.

Mwaka Mpya wa Jadi wa China ni sikukuu muhimu zaidi ya taifa la China. Sikukuu hiyo kuwa kikukuu ya Umoja wa Mataifa kunaonyesha ushawishi wa utamaduni wa China, na kutahimiza mawasiliano ya staarabu mbalimbali duniani. Vilevile pia kunaonesha wazo shirikishi la Umoja wa Mataifa kuhusu thamani ya tamaduni.

Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China ilianzishwa nchini China.  Lakini tayari imeenea duniani. Hadi sasa takriban asilimia 20 ya watu duniani wanasherehekea sikukuu hiyo, na hata baadhi ya nchi zimechukulia sikukuu hiyo kama sikukuu ya kitaifa. Kutokana na kuongezeka kwa ushawishi wa utamaduni wa Kichina, licha ya watu wenye asili ya China, watu wengine wengi wenye ustaarabu na rangi tofauti wameanza kusherehekea sikukuu hiyo.

Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China kutambuliwa na watu duniani kote pia kunatokana na juhudi za China katika kueneza na kuendeleza utamaduni wake kwa njia ya kivumbuzi. Miaka 10 iliyopita, China ilitengeneza MV kuhusu sikukuu hiyo, na kuionesha katika nchi mbalimbali, ili kuwasaidia watu duniani kufahamu utamaduni wa China.

Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China kutambuliwa na watu duniani kote pia kumethibitisha tena wazo la China la kuishi kwa pamoja kwa staarabu tofauti duniani. Katika mchakato wa urithi na maendeleo ya Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, mila nyingi za kiutamaduni za Kichina zimerithishwa. Wakati huo huo, wakati sikukuu hiyo inapoingia kwenye jukwaa la kiutamaduni duniani, imerekebishwa na watu wa nchi nyingine kulingana na utamaduni wao. Hali ambayo inaonesha kuwa Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China si ya Wachina tu, bali pia ni ya binadamu wote duniani.

Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China kuwa sikukuu ya Umoja wa Mataifa pia kunawahamasisha watu wa nchi tofauti kuchagua mawasiliano ya staarabu badala ya mivutano ya staarabu, na kuchagua kuishi kwa pamoja kwa staarabu, badala ya kujiweka mbele zaidi, ili binadamu wawe na mustakabali mzuri zaidi wa pamoja.