Ngamaleu anachukua nafasi ya Mughe katika kikosi cha Cameroon AFCON
2024-01-05 23:02:58| cri

Winga wa kikosi cha Dynamo Moscow Moumi Ngamaleu aliitwa kwenye timu ya taifa ya Cameroon siku ya Alhamisi na kocha Rigobert Song, kabla ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) itakayofunguliwa nchini Cote d'Ivoire wiki ijayo.

Ngamaleu anachukua nafasi ya Francois-Regis Mughe, ambaye alikataa kushiriki AFCON ili kuweka kipaumbele katika kuichezea klabu yake ya Marseille.

Ngamaleu, 29, alikichezea kikosi cha Cameroon kilipofika nusu fainali ya AFCON 2021 nyumbani kabla ya kuondolewa na Misri.Anatarajiwa kuungana na wachezaji wengine wa kikosi cha Indomitable Lions mapema Ijumaa mjini Jeddah, Saudi Arabia ambako timu hiyo ipo kwa sasa.