Uganda yamwomboleza mwanariadha maarufu aliyeuawa kwa kuchomwa kisu nchini Kenya
2024-01-05 08:35:07| CRI

Mke wa rais wa Uganda Janet Museveni ameomboleza kifo cha mwanariadha maarufu wa Olimpiki nchini humo, Benjamin Kiplagat, aliuawa kwa kuchomwa kisu nchini Kenya katika mkesha wa Mwaka Mpya.

Mama Museveni, ambaye pia ni Waziri wa Elimu na Michezo wa Uganda, amesema katika taarifa yake kuwa, amepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha mwanariadha huyo aliyeuawa huko Eldoret, magharibi mwa Kenya jumamosi usiku, na mwili wake kugunduliwa ndani ya gari pembezoni mwa mji huo.

Kiplagat, ambaye ni mzaliwa wa Kenya, ameiwakilisha Uganda katika mashindano mbalimbali ya kimataifa ya riadha na mashindano kadhaa ya Olimpiki.