Watu milioni 1.5 wahitaji msaada wa kibinadamu nchini Kenya
2024-01-05 08:29:17| cri

Mamlaka ya Taifa ya Kukabiliana na Ukame nchini Kenya (NDMA) jana imesema, watu milioni 1.5 nchini humo wanahitaji msaada wa kibinadamu, ambao wengi wao walikumbwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua za EI Nino za hivi karibuni.

NDMA imesema, tathmini kuhusu athari ya msimu mrefu wa mvua wa mwaka 2023 kwa chakula na usalama wa lishe, inakadiriwa kuwa idadi ya watu wanaohitaji msaada wa kibinadamu kuanzia mwezi Oktoba mwaka 2023 hadi mwezi Januari mwaka huu itapungua na kufikia milioni 1.5 kutoka milioni 2.8 ya mwezi Julai mwaka 2023.