Benki Kuu ya Tanzania kuondoa msukosuko wa dola mwaka huu
2024-01-05 14:04:38| cri

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeahidi kufanya marekebisho mwaka huu ili kutatua uhaba wa dola, na kupanga hatua za kudhibiti hali hiyo.

Hatua zinazochukuliwa ni pamoja na kuwaonya wauzaji bidhaa nje kuhakikisha kuwa mapato kutokana na mauzo ya nje yanatumwa ndani ya siku 90 za biashara, ili kuhakikisha kuna hifadhi ya kutosha ya dola katika mzunguko.

Kanuni ya Fedha za Kigeni ya 2022, inahitaji kwamba msafirishaji ahakikishe kuwa mapato kutokana na mauzo ya nje yanalipwa ndani ya muda wa siku 90 baada ya kuuza, lakini katika baadhi ya nyakati malipo yamekuwa yakichukua hadi mwaka mmoja.