Deni la Marekani lazidi kuongezeka, na kutishia uchumi wa Marekani
2024-01-05 08:19:57| CRI

Kufikia Januari 2, jumla ya deni la serikali ya Marekani lilizidi dola za kimarekani trilioni 34 kwa mara ya kwanza. Hii ni miezi mitatu na nusu tu baada ya deni la Marekani kuzidi dola za kimarekani trilioni 33, miaka mitano mapema kuliko ilivyotabiriwa na Ofisi ya Bajeti ya bunge la Marekani

Mashirika husika ya Marekani yamesema, deni hilo linazidi 120% ya Pato la Taifa la Marekani, ambayo ina maana kwamba kila Mmarekani anabeba deni la dola za kimarekani laki 1. Shinikizo hili ni kubwa sana kwa uchumi na jamii ya Marekani.

Je, deni kubwa la namna hii lilitokeaje? Wataalamu husika walisema ili kuchochea ufufukaji wa uchumi, serikali ya Marekani ilitoa deni mara kwa mara, na kusababisha deni kukua kwa kasi kuliko ilivyotarajiwa. Ili kukabiliana na mfumuko wa bei, Kamati ya Hazina ya Marekani imeendelea kuongeza viwango vya riba, na hivyo kuongeza gharama za ulipaji wa deni la serikali ya Marekani. Aidha, kuongezeka kwa matumizi ya serikali na kupunguza mapato ya kodi pia kumezidi ukubwa wa deni.

Wachambuzi wanatabiri kwamba serikali ya Marekani itaongeza deni lake kwa zaidi ya dola trilioni 2 kwa mwaka. Kwa kufikiria misimamo tofauti ya vyama viwili vya Marekani kuhusu masuala ya fedha na msimamo wa serikali wa kutochukua hatua yoyote kutatua deni lake, tatizo la deni la Marekani huenda litazidi kuwa mbaya.

Deni la nje huchangia sehemu kubwa ya deni la serikali ya Marekani. Deni la Marekani limeongezeka zaidi na hatari ya kulipia imeongezeka, jambo ambalo bila shaka litaathiri imani ya wawekezaji wa kigeni katika uchumi wa Marekani. Wawekezaji wakipunguza umiliki wao wa deni la Marekani, thamani ya dola ya Marekani itakabiliwa na shinikizo la kushuka, na hali hii itazidisha mzigo wa serikali ya Marekani wa kulipa deni lake.

Vyama viwili vya Marekani vikiendelea kuchuana vikali kuhusu masuala ya bajeti kwenye bunge la Marekani, serikali ya Marekani huenda itasimamisha kazi tena na yatadhuru maslahi ya watu wa kawaida wa Marekani mwishowe.