Sudan yamwita nyumbani balozi wake nchini Kenya kupinga nchi hiyo kumpokea kiongozi wa RSF
2024-01-05 08:35:44| CRI

Sudan jana imemwita nyumbani balozi wake nchini Kenya kupinga nchi hiyo kumpokea rasmi kiongozi wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo.

Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan Ali Al-Sadiq amesema katika taarifa yake kuwa, Kenya imesahau ukiukwaji mkubwa uliofanywa na vikosi vya waasi, na uharibifu waliofanya kwa miundombinu ya nchi hiyo na mali za wananchi wake.

Jumatano wiki hii, Rais wa Kenya William Ruto alimpokea Jenerali Dagalo mjini Nairobi, ikiwa ni sehemu ya ziara ya nje ya Jenerali huyo ambayo ilihusisha nchi za Uganda, Ethiopia na Djibouti.