Tanzania yarekodi mwaka wenye joto zaidi kuwahi kutokea
2024-01-05 14:05:08| cri

Mwaka 2023 umeweka rekodi ya kuwa mwaka wenye joto kali zaidi katika historia ya Tanzania, kutokana na kuongezeka kwa joto katika hali ya kutisha.

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imethibitisha hilo baada ya kuchambua mwenendo wa hali ya joto nchini kote, na kuona kuwa kulikuwa na ongezeko la kutisha la nyuzi joto 1.00 ikilinganishwa na miaka iliyopita.

Mamlaka hiyo imetaja sababu mbili za kuongezeka kwa joto hilo kuwa ni jua kuwa utosini, na upungufu wa mvua katika baadhi ya maeneo vimeongeza joto. Imesema kwa kawaida, jua huwa kali mara mbili kwa mwaka - wakati linaelekea kusini mwezi Novemba na wakati linaelekea kaskazini mwezi Februari.