Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant amesema jana Alhamisi kuwa, Wapalestina wataongoza masuala ya kiraia katika Ukanda wa Gaza, huku Israel ikidumisha udhibiti wa usalama wa eneo hilo baada ya mapambano ya sasa kumalizika.
Bw. Gallant amesema, hakutakuwa na raia wa Israel katika ukanda wa Gaza baada ya malengo ya vita ya sasa kutimizwa, na pia amesisitiza kuwa Israel haitaruhusu kundi la Hamas kutawala Gaza au kuhatarisha usalama wa waisraeli, kwa hivyo itabaki na uhuru wa kuchukua hatua huko Gaza.
Waziri huyo amesema Israel inaingia kwenye kile alichokiita kipindi cha tatu cha mapambano, ambacho kitahusisha mashambulizi, uharibifu wa mahandaki ya magaidi, shughuli za angani na ardhini, na operesheni maalumu.