Umoja wa Afrika wataka utulivu ili kupunguza mvutano unaoendelea kati ya Ethiopia na Somalia
2024-01-05 14:05:33| cri

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Balozi Moussa Faki Mahamat, ametoa wito wa utulivu na kuheshimiana ili kupunguza mvutano unaoendelea kati ya serikali ya Ethiopia na Somalia, kufuatia kusainiwa kwa makubaliano ya kufikia bandari kati ya Ethiopia na Somaliland.

Somaliland ina hadhi yenye utatanishi ambayo kimataifa inatambulika kuwa ni sehemu ya serikali ya Somalia. Balozi Mahmat ametoa angalizo hilo kwenye taarifa yake aliyoitoa januari 3.

Makubaliano hayo yalisainiwa Januari 1, na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed na kiongozi wa Somaliland Muse Bihi Abdi.