Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC yasikiliza ripoti za kazi
2024-01-05 14:07:03| cri

Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) tarehe 4 Januari ilifanya mkutano na kusikiliza ripoti mfululizo za kazi.

Ripoti hizo za kazi zinatoka Bunge la Umma la China (NPC), Baraza la Serikali ya China, Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC), Mahakama Kuu ya China, Idara Kuu ya Kuendesha Mashtaka ya China, na Sekretarieti ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikoumisti cha China (CPC).

Katibu mkuu wa Kamati Kuu ya CPC Xi Jinping aliendesha mkutano huo na kutoa hotuba muhimu.