Wajibu wa wanahabari wanawake katika jamii
2024-01-06 09:30:47| CRI

Wanawake wanachukuliwa kama sehemu muhimu katika jamii, na wanabeba majukumu makubwa katika jamii, ikiwa ni kuanzia ngazi ya familia na ngazi nyingine nyingi. Lakini wanawake haohao wamekuwa wakinyimwa haki zao na hata kufanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia katika kutekeleza majukumu yao ama ili waweze kupata fursa fulaniulanikatika sekta ya biashara ama katika sehemu za kazi.

Wanawake katika sekta ya habari nao pia wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali katika kutimiza majukumu yao, lakini wamekuwa wakijitahidi, bila kujali kadhia wanazokumbana nazo, kutimiza wajibu wao kwa jamii. Tumeona waandishi wanahabari wanawake wakiandika habari mbalimbali kuhusu matatizo katika jamii, lakini katika kutekeleza majukumu yao, bado pia wamekumbana na changamoto mbalimbali. Kipindi chetu cha leo cha Ukumbi wa Wanawake tutazungumzia wanahabari wanawake na wajibu wao katika jamii. Ni mambo gani wameyafanya, wanayafanya, na wamepanga kufanya ili kupunguza matatizo katika jamii.