Umoja wa Mataifa wakaridia kasi ya ongezeko la uchumi duniani kupungua mwaka 2024
2024-01-06 22:03:49| cri

Ripoti ya hali na matarajio ya uchumi duniani ya mwaka 2024 iliyotolewa jana na Umoja wa Mataifa, inakadiria kuwa ongezeko la uchumi duniani litapungua kutoka asilimia 2.7 za mwaka 2023 na kuwa asilimia 2.4 kwa mwaka 2004.

Ripoti hiyo inasema biashara dhaifu ya kimataifa, gharama kubwa za kukopa, madeni ya umma yanayoongezeka, uwekezaji unaoendelea kupungua na hali ya wasiwasi ya siasa za kijiografia vimesababisha ongezeko la uchumi duniani kukabiliwa na hatari.