Zaidi ya wanafunzi milioni 10 kunufaika na mradi wa maktaba ya mtandao Tanzania
2024-01-08 08:34:52| CRI

Zaidi ya wanafunzi milioni 11 na walimu laki 2 katika shule za umma za Tanzania watanufaika na mradi mpya wa maktaba ya mtandao nchini humo.

Mradi huo umeratibiwa na Taasisi ya Elimu ya Tanzania (TIE) kwa kushirikiana na kampuni ya Snapplify yenye makao makuu nchini Afrika Kusini inayojishughulisha na teknolojia ya elimu.

Ofisa mahusiano wa kampuni ya Snapplify, Stephen Bestbier amewaambia wanahabari mjini Dar es Salaam kuwa mradi huo unalenga kuleta mabadiliko kwenye sekta ya elimu kwa kuwezesha upatikanaji wa raslimali za elimu bora kote nchini, akiongeza kuwa mradi huo ni miongoni mwa miradi mkubwa zaidi ya elimu ya kidijitali katika bara la Afrika. Mradi huo utanufaisha shule zaidi ya 19,000 za serikali ndani ya miaka mitatu.