Rais wa Somalia abatilisha mkataba wa bandari ya Ethiopia na Somaliland
2024-01-08 08:35:32| CRI

Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia amebatilisha makubaliano yaliyofikiwa kati ya Ethiopia na Somaliland ambayo yangeiwezesha Ethiopia kufikia bandari ya Berbera, kwa mabadilishano na kuitambua Somaliland.

Rais Mohamud amesema alisaini sheria iliyopitishwa na mabaraza mawili ya bunge la nchi hiyo ya kubatilisha "Mkataba haramu wa Maelewano" uliosainiwa Januari 1, ili kuipatia Ethiopia haki ya kutumia bandari ya Bahari Nyekundu ya Berbera, hatua ambayo imetajwa na Somalia kuwa ni ukiukaji wa mamlaka yake na eneo lake, na kuiomba jumuiya ya kimataifa kuingilia kati.

Rais alisema katika taarifa yake aliyoitoa mjini Mogadishu kwamba hatua hiyo inaonyesha dhamira ya kulinda umoja, mamlaka na ukamilifu wa ardhi ya Somalia.