Wanajeshi wawaua wanamgambo 76 wa al-Shabaab katikati mwa Somalia
2024-01-08 08:49:42| CRI

Maofisa wa Somalia wamesema jeshi la taifa la Somalia (SNA) likiungwa mkono na washirika wa kimataifa limewaua wanamgambo 76 wa kundi la al-Shabaab na kuwajeruhi kadhaa kufuatia operesheni ya siku mbili katika eneo la Mudug katikati mwa Somalia.

Mkuu wa jeshi la Somalia Bw. Ibrahim Sheikh Muhidin amesema makamanda wakuu wa kundi la al-Shabaab ni miongoni mwa watu waliouawa wakati wa mashambulizi yaliyofanyika Jumamosi na mapema Jumapili.

Ameongeza kuwa mashambulizi pia yaliharibu kambi na magari ya al-Shabaab, na wanajeshi walikuwa wanapiga hatua katika kuwatokomeza wanamgambo hao kutoka kwenye ngome zao katikati na kusini mwa Somalia.