Wachimbaji 15 walionaswa mgodini nchini Zimbabwe waokolewa
2024-01-08 08:48:52| CRI

Ripoti ya Gazeti la Herald la Zimbabwe imesema wachimbaji 15 walionaswa mgodini waliokolewa Jumapili iliyopita kufuatia kuporomoka kwa mgodi mmoja wa dhahabu nchini humo.

Wachimbaji hao walinaswa asubuhi ya Alhamisi iliyopita wakati mgodi wa Redwing huko Penholonga, kilomita 265 mbali na mji wa Harare, uliporomoka kutokana na kinachohisiwa kuwa ni tetemeko la ardhi. Baadaye teknolojia ya setilaiti ilitumiwa kuhakikisha mahali wachimbaji walipo na shimo likatobolewa kuweka njia ya kuwatoa.