Miss Namibia autaka urais
2024-01-08 14:33:14| cri

Mshindi wa taji la Miss Namibia mwaka 2022, Cassia Sharpley ametangaza nia ya kugombea urais wa taifa hilo licha ya kuwa na umri mdogo (24).

Cassia Sharpley amewaambia wafuasi wake wa Instagram kwamba hivi karibuni ataanza kushiriki “safari yake ya kuwa Rais wa Jamhuri ya Namibia”.

Ingawa wafuasi kadhaa walisema kwamba wagombea urais lazima wawe na zaidi ya miaka 35, kwa mujibu wa katiba ya Namibia ila Sharrley alirudia kauli yake siku ya Alhamisi kwamba atatimiza hilo. Akiendelea kusisitiza zaidi, mrembo huyo ameahidi kuja na taarifa zaidi kuhusu namna ya kuanza harakati hizo.