Rais wa Nigeria amsimamisha kazi waziri kwa kashfa ya fedha
2024-01-09 08:27:38| CRI

Rais Bola Tinubu wa Nigeria amemsimamisha kazi waziri wa masuala ya kibinadamu na uondoaji umaskini Bwana Betta Edu, kutokana na matumizi ya fedha yenye utatanishi yaliyofanywa na ofisi yake.

Msemaji wa Rais wa Nigeria amesema kwenye taarifa kuwa kusimamishwa huko kumeanza mara moja ili kuruhusu uchunguzi wa kina kufanywa na mamlaka ya kupambana na ufisadi. Taarifa imeongeza kuwa hatua hii inaendana na ahadi ya rais ya kuzingatia viwango vya juu zaidi vya uadilifu, uwazi na uwajibikaji.

Bw. Edu alikosolewa vikali baada ya kudaiwa kuamuru kuhamisha zaidi ya naira milioni 585.2 (zaidi ya dola za Kimarekani 661,374) zilizokusudiwa kulipwa kwa raia "walio katika mazingira magumu" kwenye akaunti ya benki ya kibinafsi ya mtumishi wa umma.