OCHA: Usambazaji wa misaada ya kibinadamu nchini Sudan unakumbwa na changamoto mbalimbali
2024-01-09 09:00:13| CRI

Ofisi ya Uratibu wa Masuala ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) imesema usambazaji wa misaada ya kibinadamu katika maeneo mengi nchini Sudan umekumbwa na changamoto mbalimbali, ikiwemo kukosekana kwa usalama na ukosefu wa pesa taslimu, uporaji, urasimu, mawasiliano duni ya mtandao na simu na ukosefu wa wafanyakazi wa kibinadamu na kiufundi.

Pia OCHA imeongeza kuwa ukosefu wa nishati pia umeleta taabu kwa kazi hiyo ya usambazaji pamoja na uzalishaji wa umeme kwa ajili ya uhifadhi wa mnyororo baridi na usambazaji wa maji.

Licha ya hayo OCHA imesema hadi kufikia Januari 4 mwaka huu, mpango wa misaada ya kibinadamu wa 2023 kwa Sudan uliorekebishwa ulifadhiliwa kwa asilimia 40.8 tu.