UM walaani mauaji ya raia 28 wakati wa uvamizi wa mifugo nchini Sudan Kusini
2024-01-09 08:30:13| CRI

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS) umelaani ghasia zilizosababisha vifo vya raia 28 wiki iliyopita katika Kaunti ya Duk ya Jimbo la Jonglei.

Mamlaka ya Jimbo la Jonglei imehusisha shambulio hilo ambalo pia limesababisha takriban watu 19 kujeruhiwa, na vijana wa kabila la Murle waliokuwa na silaha kutoka eneo jirani la Utawala la Greater Pibor.

UNMISS imetoa wito kwa pande zote zinazohusika kusitisha mashambulizi ya kulipiza kisasi, na kutumia njia za amani kutatua malalamiko yao.

Ujumbe huo pia umeitaka serikali ya jimbo la Jonglei na mamlaka ya eneo la Utawala la Greater Pibor kufanya mazungumzo na kuwafikisha wahusika mbele ya sheria, na kuzuia unyanyasaji.